Nateseka(pain)

By youngsta soldier •
Nikiandika hii stanza moyo wangu unavunja
Chuki nayohisi ni nyingi siwezi kuikunja
Mawazo yananisumbua akili
Mawazo yananichangamsha
Ni kama nimewekwa gizani
Ni kama nimeshinda na njaa
Nashinda siku hii itanipeleka wapi
Kushoto,Kulia nifuate njia gani?
Sina chochote ila imani
Kwako Mola Kwani wewe ndiyo mkuu
Usiku,mchana kila kitu iko kawa
Nakuuliza Mola wangu unipe mabawa
Ilili ni pepee kama ndege
Hadi upeoni kama mwewe
For those of you who dont understand Swa this poem is about pain and hardships.I'm asking God to give me wings to fly away from my troubles.